Maagizo Rahisi ya PasakaHili ni toleo rahisi la Pasaka iliyofuatwa na ufafanuzi kuhusu vikombe vinne vya divai na kikombe cha Eliya.Hatua I: Ondoa chachu kutoka kwa nyumba au chumba chako kama unaishi na wazazi au wengine wasiosherehekea. Hii inamaanisha kuwa uondoe mikate iliyo na chachu, biskuti, crackers, chochote kilicho na chachu kama baking soda au baking powder. Chachu ni ishara ya dhambi na upotovu. Angalia 1 Wakorintho 5:6-8.Hatua II: Maandalizi – Utakachohitaji

 • Yai lililochemshwa; hili ni kumbusho la dhabihu ya Hekalu ya Sikukuu na pia ishara ya maisha. Ilitolewa pale kwa Hekalu wakati wa Sherehe ya Pasaka, Pentekoste na Vibanda. (Kumbukumbu la Torati 16:16)

 • Mwanakondoo; nyama hii na mfupa wake ni makumbusho ya Dhabihu ya Hekalu na Mwanakondoo wa kwanza wa Pasaka.

 • Mfupa wa mwanakondoo

 • Mimea chungu (horseradish)

 • Mboga: Parsley, vipande vya lettuce

 • Maji ya chumvi

 • Charoset, inayowakilisha ‘mortar’ ambayo watumwa pale Misri walitumia kujenga miji ya farao

 • Matzah au crackers zisizo na chachu kama ‘Ryvita’

(Kwa charoset, changanya nusu ya tufaha zilizokatwakatwa katika vipande, kijiko kidogo cha njugu zilizokatwa, divai kidogo au sharubati ya zabibu, kijiko kidogo cha mdalasini.)

 • Divai au sharubati ya zabibuHatua III: Seder ya Pasaka (inatamkwa kama “say dar” – inamaanisha “mpangilio”)

 • Anza Seder na maombi ya kumshukuru BABA YAHUVEH wa Mbinguni kwa yote YEYE Amefanya kwa ajili yetu na Atafanya kwa ajili yetu, Watoto WAKE, Anapotulinda na kutuchunga kupitia majaribu mengi ya maisha na kwa MWANA WAKE YAHUSHUA MASIHI wetu na BWANA ARUSI wetu Ajaye, kwa Wokovu Aliotupa pale Kalvari na kwa IMMAYAH, MAMA yetu wa Mbinguni Anayetuchunga sisi na kutuongoza katika kila nyayo tunayochukua kama tu tutatii.

 • Mwaga kikombe cha divai au sharubati ya zabibu na sema Baraka juu yake. Kwa mfano: “Ubarikiwe EWE BABA YAHUVEH, BABA wetu wa Mbinguni na MUUMBA wa tunda la mzabibu. WEWE Umetufanya sisi Watakatifu kupitia Damu iliyomwagwa ya MWANA WAKO YAHUSHUA MASIHI wetu. Umetufikisha salama hapa tulipofika na tunakushukuru WEWE kwa kutuongoza kila siku ya maisha yetu. Tunakupa WEWE Sifa, Heshima na Utukufu wote, sasa na milele! Baraka kwa Jina la YAHUVEH MUNGU MWENYEZI! Jina la YAHUSHUA MASIHI na IMMAYAH, MAMA SHKHINYAH GLORY, RUACH HA KODESH wetu Mpendwa, MALKIA wa pekee wa Mbinguni!” (Tafadhali ongeza maombi yako.) Kunywa divai au sharubati ya zabibu.

 • Osha mikono

 • Tumbukiza parsley kwenye maji ya chumvi na kula ukieleza kuwa maji haya ya chumvi yanatukumbusha machozi ya Wayahudi waliyolia kule Misri na zile mboga ni ishara ya kuja kwa Msimu wa Machipuko inayoleta tumaini.

 • Kula matzah, ukieleza kuwa matzah, au mkate usio na chachu ni kumbusho la jinsi Wayahudi walivyoacha misri kwa haraka usiku wa Pasaka.

 • Kula mimea chungu, horseradish. Huwa wakati mwingi kipande cha mboga hutumbukizwa au kipande cha matzah hutumbukizwa kwenye horseradish, alafu huliwa. Haya yanatukumbusha jinsi Wamisri walivyohuzunisha au kufanya machungu, hayakubaliki, maisha ya Wayahudi ambao pia ni sisi kwa kuwa tumeunganishwa kwenye mzabibu kupitia YAHUSHUA. (Warumi 11:17-19) Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, walifanya kazi zote za mashambani na katika kazi zao zote ngumu Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili. (Kutoka 1:14)Hatua IV: Soma kwa sauti ya juu Hadithi ya Pasaka, Kutoka 10-15.

Kimila, chakula cha Pasaka cha nyama ya mwanakondoo huliwa wakati huu. Sio lazima lakini.Hatua V: Yai lililochemshwa: Yai lililochemshwa linaliwa sasa hivi, likitumbukizwa katika maji ya chumvi. Linaweza kulwa pale mwanzoni wa Pasaka au pekee yake kama hautakula chakula. Yai lililochemshwa ni ishara ya mateso na ukandamizaji kule Misri. Kila kitu kingine kwa maji moto huwa laini au kuvunjikavunjika lakini yai huwa ngumu kama Wanaisraeli. Ikichemshwa zaidi, inazidi kuwa ngumu. Yai pia huwa ishara ya maisha mapya.

Kwa kuongeza, YAHUVEH Amefunua kwake Elisabeth kuwa sehemu 3 za UTATU ni kama yai – kila sehemu ni tofauti na bado ni sehemu ya yote. Kama BABA YAHUVEH Alivyosema kwake Elisabeth, “Ni sehemu gani la yai ambalo ni yai? Je, ni ganda? Albumen (sehemu nyeupe) au kiini cha yai?” Bila shaka ni yote tatu – kila sehemu tofauti na bado kila sehemu ikiwa sehemu ya yote, yai lote. Ni ya ajabu, au sio?Hatua VI: Soma kwa sauti ya juu Zaburi 126, Nyimbo ya sherehe na ushindi…

Wapandao kwa machozi, watavuna kwa kelele za furaha!...” Asante EWE BABA YAHUVEH kwa ushindi juu ya vitu vyote maishani mwetu ambayo si ya KWAKO katika Jina la YAHUSHUA MASIHI wetu!* * * * * * *

Vikombe 4 vya DivaiKimila, katika Seder ya Pasaka vikombe vinne vya divai au sharubati ya zabibu hutumika katika Seder lakini haijaamrishwa na YAHUVEH. Vikombe hivi vinne huwa ishara ya aina 4 ya ukombozi BABA YAHUVEH Anayotumia Akielezea kutoka kwa Wayahudi kule Misri kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Kutoka 6:6-7:

YAHUVEH Anasema:

 1. Nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri...”

 2. Nitawaweka huru mtoke katika kuwa watumwa wao…”

 3. Nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa…”

 4. Nitawatwaa mwe watu WANGU mwenyewe, Nami Nitakuwa MUNGU wenu…”

Kimila, pia kuna kikombe cha tano cha divai kiitwacho, “Kikombe cha Eliya.” Kikombe hiki hujazwa tu lakini hakitumiki na mlango unafunguliwa katika matarajio ya kuja kwa Nabii Eliya kutangaza MASIHI, MASHIACH, YAHUSHUA.

Nabii Eliya anafikiriwa kuwa anayeleta habari njema za furaha na amani. Jina la Eliya linahusishwa na kuja kwa MASIHI, ambaye kuja kwake, Eliya anatarajiwa kutangaza.

Tunasoma: “Tazama, Nitawapelekea Nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya BWANA. Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo Nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.’’ (Malaki 4:4-6a)

Mila ya Kiyahudi husema kuwa Eliya hutembelea kila nyumba ya Myahudi wakati wa Seder na hunywa kwenye kikombe. Wakati Israeli ilipokuwa katika utumwa walipohamishwa kutoka nchi yao, kikombe cha Eliya kilijazwa, lakini hakikutumika. Huwa kinabaki kama ishara ya ahadi ya Kimasihi ya BABA YAHUVEH ya upya.

YAHUSHUA Alisema kuhusu Yohana Mbatizaji kwenye Kitabu cha Marko 9:11-13 & Mathayo 11:13-14,

Wakamwuliza, ‘Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?’ YAHUSHUA Akawajibu, ‘Ni kweli, Eliya yuaja kwanza, ili kurudisha upya mambo yote. Mbona basi imeandikwa kwamba MWANA wa MUNGU ni lazima Ateseke sana na kudharauliwa? Lakini Ninawaambia, Eliya amekwisha kuja nao wakamtendea walivyopenda, kama ilivyoandikwa kumhusu yeye.’’’

Kwa maana Manabii wote na Torati vilitabiri mpaka wakati wa Yohana. Kama mko tayari kukubali hilo, yeye Yohana ndiye yule Eliya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. Yeye aliye na sikio na asikie.”

Eliya amekuja” – Haya yalikuwa kweli kwa utu wa Yohana Mbatizaji aliyekaribisha kuja kwa YAHUSHUA Alipokuja duniani miaka 2000 iliyopita.